Home » » Club olympia ya sinza-mori yateketea kwa moto

Club olympia ya sinza-mori yateketea kwa moto

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, January 28, 2015 | 1:14 PM


 
 
 
 


Askari wa zima moto wakinyoosha mipira ya maji

CLUB  Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.
 Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel  Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.
Aliongeza kwamba zima moto  hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako  saa 12 asubuhi wakiwa na maji  kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.
(Picha na Denis Mtima/GPL).

0 comments :

Post a Comment