Home » » Asaula akimfuta jasho bi. Harusi

Asaula akimfuta jasho bi. Harusi

Written By Bewith Jeddy on Friday, January 2, 2015 | 8:18 AM

 Mwanamke huyo akisahula wakati anamfuta jasho bibi harusi.

HII aibu ya kufungulia mwaka wa 2015! Mwanamke mmoja ambaye inadaiwa ni mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la Mishi Choggo ametoa kali ya mwaka baada ya kusaula kisha kutumia gauni lake kumfutia jasho bi. harusi.
Bi’mkubwa huyo alifanya kioja hicho Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Rose Garden maeneo ya Mafinga mkoani hapa katika harusi ya Rose Raphael na Edward Sebastian ambao
walikuwa wakibariki ndoa.Wakati sherehe ikiwa imepamba moto na waalikwa mbalimbali wakianza kutoa zawadi, mama huyo alimfuata DJ na kuomba awekewe wimbo wa taarabu, akaanza kucheza kwa madaha huku akienda kutunza.
Huku paparazi wetu akifotoa picha hatua kwa hatua, mama huyo alipomkaribia bibi harusi, alisaula gauni lake refu na kulitumia kumfuta jasho bi. harusi baada ya kukosa hanjifu.Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu wanaojiheshimu kuinamisha vichwa chini kwa aibu huku wale micharuko wenzake wakishangilia.
Mama huyo akizidi kijichetua.
“Huyu si bure atakuwa amezidisha kilevi na matukio ya namna hii siku hizi si mazuri maana anaharibu shughuli ya watu, watu tunapaswa kubadilika. Yaani kweli amekosa hanjifu ya kumfutia jasho bi. harusi mpaka afanye vile?” alihoji mmoja wa waalikwa.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment