Home » » Zitto amtambulisha mchumba wake KIGOMA

Zitto amtambulisha mchumba wake KIGOMA

Written By Bewith Jeddy on Wednesday, December 3, 2014 | 2:38 PMMBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake
mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni. Mchumba huyo
Utambulishio huo wa mchumba wa Zitto ulifanywa na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) wakati wa sherehe ya Harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex.
hali ilikuwa hivi; baada ya Kafulila kutambulisha ndugu zake pamoja na wazazi wake ndipo alianza kutambulisha wageni wengine na kuanza na mchumba mtarajiwa wa Zitto Kabwe aliyemtaja kwa jina la Anna.
“Huyu wa kwanza anaitwa Anna anafanya kazi Ubalozi wa Ireland ni mchumba mtarajiwa wa Zitto Zuberi Kabwe, anayefuata kutoka kushoto kwa Anna wote mnamfahamu ndiyo Zitto mwenyewe na anayemfuata ni Mwalimu wangu wa chuo kikuu Kitila Mkumbo na mwisho ni mbunge mwenzangu David Silinde hao ndo walio nisindikiza,” alisema Kafulila

0 comments :

Post a Comment