Home » » Waliomuua Aisha Madinda wasakwa!

Waliomuua Aisha Madinda wasakwa!

Written By Bewith Jeddy on Monday, December 22, 2014 | 8:50 AM

 Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake.

Kimenuka! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, zilidai kwamba
jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana.
“Aisha alipofikishwa Mwananyamala alikuwa ameshafariki dunia. Sasa waliokuwa naye wanajua aliyehusika kwa namna yoyote ile lazima wakamatwe,” kilisema chanzo cha ndani cha jeshi hilo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
 Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.

Ili kupata undani wa ishu hiyo, Jumamosi iliyopita Ijumaa Wikienda lilizungumza na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
Aisha (35) alizikwa Ijumaa iliyopita huko Kigamboni, Dar, baada ya kukutwa na umauti wa kutatanisha Jumatano ya wiki iliyopita.

Source: GPL


0 comments :

Post a Comment