Home » » Ndoa sasa yamzeesha Maimartha

Ndoa sasa yamzeesha Maimartha

Written By Bewith Jeddy on Friday, December 19, 2014 | 9:13 AMStori: Hamida Hassan
Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha yeye kuingia kwenye maisha ya ndoa kimemsababisha sasa aonekane kama aliyezeeka kwani mambo mengi ya kisichana ameyaacha.Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’.
Akizungumzia maisha anayoishi Mai alisema, zamani alikuwa ikifika wikiendi anafikiria akajirushe wapi lakini sasa hivi imebaki historia kiasi cha baadhi ya mashosti zake kumtania kwa
kumwambia, hana nyimbo na amezeeka.
“Kama ni suala la ndoa kunizeesha kweli imenizeesha, sasa hivi siyo yule Mai wa kila wikiendi kwenda kula bata, wapo mashosti ambao wananiponda kwa kubadilika kwangu lakini sijali, unajua kila jambo lina mwisho,” alisema Mai.

0 comments :

Post a Comment