Home » » Madai mazito: Aaunt anasa mimba nje ya ndoa

Madai mazito: Aaunt anasa mimba nje ya ndoa

Written By Bewith Jeddy on Friday, December 5, 2014 | 10:57 AM

 Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa viwanja na shosti yake, Wema Sepetu.Madai mazito! Pamoja na kutumia nguvu kubwa kukanusha kwa miezi kadhaa, bado staa wa
sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, anaendelea kugandwa na madai kwamba, amenasa mimba nje ya ndoa, Ijumaa lina mkanda kamili.


Habari hizo zilishika kasi mithili ya moto wa kifuu baada ya Aunt kunaswa Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.
KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.
WEMA ADAIWA KUMSINDIKIZA KLINIKI
Kwa mujibu wa mpenda ubuyu wetu ambaye naye alikuwemo ukumbini humo, kwa kumtazama Aunt anaonekana kuwa na ujauzito wa si chini ya miezi minne sasa na kwamba Wema ambaye ni shosti wake anadaiwa kuwa huwa anamsindikiza kliniki lakini staa huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana.
UJAUZITO MIEZI MINNE
“Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:


 Aunt Ezekiel akiwa na dansa wa 'Diamond', Mose Iyobo.

“Mwanamke mjamzito anajulikana kabisa. Hebu mcheki usoni alivyobadilika. Yaani kawa mweupe wakati Aunt huwa ana rangi ya chokuleti. Ukweli ni kwamba ana dalili zote za kubeba mimba.”
MAKE-UP YAMKATAA
Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kwamba, siku hiyo, Aunt hakuwa amechangamka kama alivyozoeleka siku zote na uso wake ulionekana kama mtu aliyechoka na hata ‘make-up’ aliyoweka haikuwa ikionekana vizuri.
NDUGU WAANZA MANENOMANENO
Habari zaidi zilidai kwamba, baadhi ya ndugu na mawifi wa staa huyo wameanza kucharuka wakidai kwamba Aunt atakuwa amepata ujauzito huo nje ya ndoa kwa kuwa muda mrefu hajaonana na mumewe, Sunday Demonte anayedaiwa kuwa gerezani huko Dubai.“Tangu mumewe apate matatizo Dubai hawajaonana hivyo Aunt hawezi kusema ni ya mumewe,” kiliendelea kudai chanzo chetu.
VITABU VYA DINI
Baadhi ya ndugu hao wametaka vitabu vya Dini ya Kiislam viweke wazi kama ni sahihi kwa Aunt kubeba ujauzito nje ya ndoa kwani kwa upande wao wanapinga kitendo hicho na kwamba ni udhalilishaji kwa ndugu yao ambaye alifuata taratibu zote za kumuoa staa huyo.Aunt Ezekiel wakati wa kufunga ndoa.
MNENGUAJI WA DIAMOND AHUSISHWA
Sosi huyo alidai kwamba ujauzito wa Aunt unahusishwa na mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moze Iyobo ambaye kwa sasa wamegandana kama kumbikumbi wakisemekana kuwa kwenye mahaba niue.
SHEHE ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata huku likijiridhisha kuwa Aunt anakaribia miaka miwili bila kukutana na mumewe, gazeti hili lilizungumza na Shehe Kaima wa jijini Dar ambaye analijua vizuri sakata la staa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada ya ndoa, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka.
“Ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena.”
AUNT ANASEMA?
Kama alivyojitetea siku ya bethidei yake oktoba, mwaka huu baada ya kuvaa kigauni cha pinki kilichoonesha kitumbo kikianza kuchomoza, katika tukio hilo la Jumapili iliyopita, Aunt ameendelea kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
“Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa,” alisema Aunt kwa kifupi.
MIAKA MIWILI ILIYOPITA
Oktoba 18, 2012, Aunt alifunga ndoa na Sunday ambapo mwigizaji huyo alibaki huku mumewe akitimkia Dubai kabla ya baadaye kupata matatizo na kutupwa jela.

Source: GPL

0 comments :

Post a Comment