Home » » Happiness Watimanywa awashukuru WATANZANIA wote kupitia INSTAGRAM kwa support waliyompa na kumpongeza Miss South Africa aliyetwaa taji la Miss world 2014

Happiness Watimanywa awashukuru WATANZANIA wote kupitia INSTAGRAM kwa support waliyompa na kumpongeza Miss South Africa aliyetwaa taji la Miss world 2014

Written By Bewith Jeddy on Monday, December 15, 2014 | 9:22 AMBaada ya Miss South Africa anajulikana kwa jina la Rolene Strauss ambaye ndie mshindi wa taji la Miss World 2014, Aliyekuwa akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram amefunguka baada ya kushindwa kunyakua taji hilo na hichi ndicho alichokiandika

Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha.
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank you.
Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you.
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.
Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld
Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22 akiwa ni mwanafunzi wa chuo cha udaktari katika chuo kikuu cha Free State (University of Free State) Rolene alifuatiwa na mshindi wa pili amabye jina lake ni Miss Hungary Edina Kulcsar.

0 comments :

Post a Comment