Home » » PICHA ZA RECHO ZAMZUIA SAGUDA MAMBO YA MAPENZI

PICHA ZA RECHO ZAMZUIA SAGUDA MAMBO YA MAPENZI

Written By stephen kavishe on Friday, November 28, 2014 | 11:00 AM

ALIYEKUWA mchumba wa msanii wa filamu Bongo, marehemu Sheila Haule ‘Recho’,  George Saguda amefunguka kuwa picha za mwanadada huyo zimekuwa zikimfanya asiwe na hisia za kuwa na mwanamke mwingine.
George Saguda akiwa na aliyekuwa mchumba wake marehemu Sheila Haule ‘Recho’.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, Saguda alisema tangu mchumba wake huyo afariki dunia hajawahi kuwa na mwanamke na hana mpango huo kwa sasa labda hapo baadaye.

“Tangu alipofariki Recho niko peke yangu na sina mpango wa kuwa na mwanamke mwingine, kwani kila ninapozitazama picha zake naumia sana,” alisema Saguda.
Saguda aliongeza kuwa, licha ya kwamba yeye ni  mwanaume aliyekamilika lakini tangu mchumba wake alipofariki dunia hana hisia za kimapenzi kwa mwanamke mwingine na akipata hali hiyo huzitazama picha zake hisia hizo hutoweka.

0 comments :

Post a Comment