Home » » DIAMOND, ZARI WAUMBUKA!

DIAMOND, ZARI WAUMBUKA!

Written By stephen kavishe on Friday, November 28, 2014 | 8:11 AM


Licha ya madai wanayoyatoa mastaa wawili hot kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady kuwa si wapenzi bali kuna project wanaifanya, wawili hao wameumbuka.
Kuumbuka huko kumekuja kufuatia kuvuja kwa picha inayowaonesha mastaa hao wakidendeka huku wakiwa kwenye hisia kali.


Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zarinah Hassan wakibusiana kimahaba.
Katika picha hizo ambazo kwa sasa zinapatikana mtandaoni, Zari anaonekana akiwa amevaa kofia ya Diamond wakionekana wenye furaha na baadaye wakahamia kwenye kupeana mahaba.

Aidha, picha ambayo inawaumbua ni ile ya kudendeka ambapo baadhi ya wadau walioiona walisema, inavyoonekana projecti wanayoifanya imevuka mipaka.

Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zarinah Hassan wakiwa kwenye pozi.
“Wasitutanie bwana, hivi kweli kwa picha hii watasema ni projekti? Hawa ni wapenzi ila hawataki tu watu wajue,” alisema mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John baada ya kuona moja ya picha hizo.
Awali, Diamond ambaye hivi karibuni alimwagana na mpenzi wake Wema Sepetu alinukuliwa akisema kuwa, watu wasidhani yeye na Zari ni wapenzi bali kuna projecti wanayoifanya.
Aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Wema Sepetu.
Licha ya madai hayo, wengi wamekuwa hawaamini kutokana na ukaribu uliopitiliza na picha zinazoendelea kuvuja huku wakisema, kama ni wapenzi bora waseme kwani wote wako singo kwa sasa.

0 comments :

Post a Comment