Home » » NDOA NDOANO:MKE AMWAGIA MUMEWE MAJI YA MOTO BAADA YA KUULIZWA NA MUMEWE KWANINI AMECHELEWA KURUDI NYUMBANI!!

NDOA NDOANO:MKE AMWAGIA MUMEWE MAJI YA MOTO BAADA YA KUULIZWA NA MUMEWE KWANINI AMECHELEWA KURUDI NYUMBANI!!

Written By stephen kavishe on Friday, October 3, 2014 | 4:53 PM


Mwanamke mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi wilayani hapa, tukio hilo lilitokea juzi, saa 4:30 usiku, katika mtaa wa Nyamakokoto,  mjini Bunda, baada ya kuzuka ugomvi ulitokana na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) kuchelewa kurudi nyumbani.

 Mwanaume huyo amejeruhiwa vibaya mume wake sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyopelekea kulazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.
 
Akizungumza na NIPASHE juzi, mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.

Alisema siku hiyo alitoka kazini kwake saa 1:00 usiku na kukuta mke wake ambaye amezaa naye watoto wanne akiwa hajarejea nyumbani huku watoto hawajetengewa chakula.
 
Alisema baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi kurudi muda huo.

Alisema baada ya kufika saa 4:00 usiku wakati watoto wake wameshabandika maji ya kupikia ugali, aliamua kwenda kwa rafiki wa mke wake ili kuuliza alipo mkewe, lakini walisema hawajamuona.

Alisema aliamua kurejea nyumbani na ilipofika saa 4:30 usiku mwanamke huyo alirejea na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa kiasi hicho, alichukuwa sufuria la maji ya moto na kumwagia.

“Tangu nimuowe na kufanikiwa kuzaa naye watoto wanne sijawahi kumpiga licha ya kufanya vituko vya mara kwa mara….sasa aliporejea muda wa saa 4:30 na mimi kumuuliza ni kwani amechelewa kiasi hicho na akijua ni mke wa mtu, hapo ndipo alipochukuwa maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali na kunimwagia” alisema.

Mganga wa zamu katika hospitali ya Bunda, Dk. Bakari Ibrahimu, alisema majeruhi huyo amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa kifuani na mikononi na kwamba anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
 

0 comments :

Post a Comment