Home » » NDOA, HAIPO: GARDNER AMSALITI JIDE?

NDOA, HAIPO: GARDNER AMSALITI JIDE?

Written By stephen kavishe on Saturday, October 11, 2014 | 8:09 AM

LICHA ya kutothibitishwa juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa ndoa yake na mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ amenaswa na kabinti akiwa kwenye pozi tata za kimahaba hivyo baadhi ya watu kuhoji anasaliti ndoa? Risasi Jumamosi lilifuatilia hatua kwa hatua.
Mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ akiwa katika pozi la kimahaba na binti huyo.


Tukio hilo lililojaa viulizo kibao bila majibu, lilifuatiliwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hatua kwa hatua ambapo lilijiri Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar kulipokuwa tamasha la wazi la kuibua vipaji vya wasaniii mbalimbali.

Awali, vijana mbalimbali walipanda katika onesho hilo na kuonesha vipaji huku binti huyo jina halikupatikana mara moja, alionekana na rafiki yake ambapo wote walikuwa ni washiriki katika onesho hilo.
GARDNER AMUIBUKIA
Wakati mtangazaji huyo akiwa katika mizunguko yake ufukweni hapo, ghafla jicho lake lilitua kwa binti huyo na kumfuata kisha kumnong’oneza kitu (haikujulikana alimwambia nini).

Gardner na mrembo wakiwa pamoja.
Huku wapenda ‘ubuyu’ wakimfuatilia kwa ukaribu, ndani ya muda mfupi, binti huyo alionekana kuelewa mazungumzo ya Gardner kwa kutingisha kichwa kuashiria ujumbe umemfika vizuri.
WACHEPUKA
Baada ya Gardner na mrembo huyo kusikilizana, wanahabari wetu waliwashuhudia wawili hao wakishikana mikono na kuondoka eneo hilo kwenda kununua vinywaji kisha wakajitenga sehemu wakinywa vinyaji huku Gadner akiwa amemkubatia kwa nyumba mtoto huyo mzuri na mwembamba kama Jide.

WAHAMA PAMOJA
Mashushushu wetu waliwashuhudia wawili hao wakipiga misele pamoja katika maeneo mbalimbali ya ufukwe huo huku mtoto wa kike akiachia tabasamu zito huku jamaa akiwa amemzungushia mkono kiunoni, wakizungumza maneno yalioonesha kuwa wapo kwenye urafiki mzuri.

Akimnong'oneza jambo.
WAPENDA UBUYU SASA!
Wakati Gardner akiwa bize akifanya yake huku akiwa ameongeza umakini, baadhi ya watu ambao ni wepesi kufuatilia mambo ya watu (wapenda ubuyu/umbeya), walianza kuibua minong’ono kwamba kulikoni mtangazaji huyo ambaye amekuwa mzito kutamka kwamba hawako pamoja na Jide, ajiachie kiasi hicho na mrembo huyo.

“Jamani huyu si ni Gardner? Vipi tena mbona anaambatanaambatana na huyu mtoto? Kwa vyovyote ni wazi kabisa kuna kitu kinaendelea kati yao, maana muda wote wapo beneti.“Duh! Sijui Jide akiwaona katika pozi kama hizi atajisikiaje kama kweli hawajaachana,” alisikika mmoja wa wapenda ubuyu.
Baada ya wanahabari wetu kupata walakini na kutaka kuthibitisha hilo, walianza kumfuatilia hatua kwa hatua mpaka waone mwisho wa mchezo utakavyokuwa baada ya kuona dalili hizo, kwa kuwa kadiri muda ulivyozidi kwenda ndivyo mambo yalipozidi kujianika hadharani huku wakijitahidi kukwepa kamera lakini waligonga mwamba.
WABADILISHANA VINYWAJI
Kuonesha kwamba urafiki wao si wakubahatisha, kuna wakati Gardner na mrembo huyo walibadilishana vinywaji jambo ambalo lilifanyika chini ya wapambe wa Gardner ambao walikuwa wakimzingira ili mapaparazi wasiweze kupata picha kwa urahisi.

Akizidi kuwanaye bega kwa bega.
Hata hivyo, mapaparazi wetu walifanikiwa kuzipata picha hizo kwa kutumia mbinu za kiintelijensia kama zinavyoonekana katika ukurasa wa mbele.
WATOWEKA
Wakati mapaparazi wetu wakiendelea kuwafuatilia, ghafla Gardner alitoweka eneo hilo lililokuwa na watu wengi kisha baada ya muda mfupi binti naye akatokomea kusikojulikana.

JIDE AAMBIWA AJIONGEZE!
Kwa mujibu wa mashuhuda wa mpango huo, mke wa Gardner, Jide anapaswa kujiongeza ili kulinda mali yake la sivyo wasichana wa mjini watamzidi kete.

BOFYA HAPA KUMSIKIA GARDNER
Alipotafutwa Gander kupitia simu ya mkononi juzi, Alhamisi ili kuulizwa kuhusu mrembo huyo, mtangazaji huyo alikiri kuwepo Coco kwenye shoo hiyo lakini hakumbuki ni binti gani amuone vizuri kwenye picha.
“Ebwana ni kweli nilialikwa kwenye hiyo shoo so nilikuwepo lakini kuhusu kabinti siwezi kukumbuka labda nione picha.

“Kweli nilipiga picha na mabinti wengi so sijui ni yupi, unajua nature (asili) ya kazi yangu (utangazaji) nakutana na watu wengi na wanapenda kupiga picha na mimi,” alisema Gardner.
Waandishi: Mayasa Mariwata, Denis Mtima na Shani Ramadhani

0 comments :

Post a Comment