Home » » KILIO CHA VANESSA MDEE KWA WATANZANIA!

KILIO CHA VANESSA MDEE KWA WATANZANIA!

Written By stephen kavishe on Wednesday, October 1, 2014 | 10:00 AM

Vanessa Mdee ambaye yeye pamoja na Diamond Platnumz na Peter Msechu wamechaguliwa kuwania tuzo za ‘All Africa Music Awards, AFRIMA 2O14, amesema kama Watanzania watawaunga mkono wana nafasi ya kuiletea nchi sifa kubwa.Vanessa amesema kuwa muziki wake unaonesha mwanzo mzuri wa kuanza kutambulika zaidi kimataifa.
“Inaonyesha ile kazi tunayofanya kila siku tunavyoamka tunaenda studio, tunavyofanya show tunaonekana tunakubalika,” amesema Vanessa. “Kusema kweli nilivyokuwa naanza muziki nilikuwa naona nitafanya vitu vikubwa na Mungu ndo anazidi kunifungulia milango, yaani sasa hivi kila kitu kinaenda sawa. Pesa tuliyoweka kwenye muziki inaanza kurudi kama unavyoona nominations, watanzania wengi tumepata nomination Peter Msechu, Diamond and myself ndio tumepata nomination. Kusema ukweli hiki ni kitu kikubwa sana kwetu. Kwa sasa tunaendelea kuonekana watanzania kimuziki.”
“Mimi ningependelea kuendelea kupata support kutoka kwa watanzania. Ukiangalia Wanigeria wanashikana sana, Wasouth wanashikana sana, na naona Wakenya wanashikana sana kwenye mambo ya muziki wao. Kushikana lazima tushikane, kweli ninafikiria watanzania wataona umuhimu wa ku-support kazi za nyumbani, kusaidia wasanii wa nyumbani Diamond, Peter na mimi kwenye Afrima,” alisema Vee.

0 comments :

Post a Comment