Home » » KIJANA AGONGWA NA GARI MBEYA KISHA KUFARIKI PAPO HAPO

KIJANA AGONGWA NA GARI MBEYA KISHA KUFARIKI PAPO HAPO

Written By stephen kavishe on Monday, October 6, 2014 | 3:09 PM

Mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Robert Mgala (21) mkazi wa Ihanda alifariki dunia baada ya kugongwa na gari isiyofahamika namba zake za usajili lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika jina wala makazi yake. 
Ajali hiyo imetokea mnamo jana majira ya saa 16:00 jioni huko katika kijiji cha Ihanda, kata ya Ihanda, tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tunduma. Chanzo cha ajali kinachunguzwa. Dereva alikimbia mara baada ya ajali hiyo, jitihada za kumtafuta zinaendelea. 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi. Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuwa makini, kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. 
Aidha, anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo dereva aliyehusika katika ajali hii azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

0 comments :

Post a Comment