Home » » KAJALA AMSHTAKI MAMA WEMA!

KAJALA AMSHTAKI MAMA WEMA!

Written By stephen kavishe on Thursday, October 2, 2014 | 7:47 AM

KIMENUKA! Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa
Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
KUNASWA KWA SAUTI NA PICHA
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.

Wema Sepetu akiwa na mama yake.
KAJALA AAMUA ZITO
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.

Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika sana.“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Wema Sepetu akiwa na Kajala Masanja.
MATUSI YENYEWE
Katika sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki gazetini)  huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.

AGUNDUA TIMU KAJALA IMO NDANI YA BETHIDEI
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”

KAJALA SASA
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya paparazi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.

Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi na tano  alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Mama yake Wema Sepetu.
ALICHOKIFANYA MARTIN KADINDA
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao wamependana.

“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!

0 comments :

Post a Comment