Home » » JACK CHUZ: ETI MUME ANIZUIE KUIGIZA, ANAANZAJE!

JACK CHUZ: ETI MUME ANIZUIE KUIGIZA, ANAANZAJE!

Written By stephen kavishe on Thursday, October 9, 2014 | 10:30 AM

STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ amefunguka kuwa madai yaliyozagaa kuwa mumewe, Gadna Dibibi amemzuia kuigiza hayana ukweli kwani naye anapenda kumuona runingani.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ akiwa na mume wake Gadna Dibibi.
Jack alifunguka hayo alipokuwa akijibu swali la paparazi wetu lililodai kuwa mume wake
amempiga mkwara asiigize kutokana na wivu.
“Wee, eti anizuie kuigiza anaanzaje kwanza? Mume wangu alinikuta niko katika kazi hiyo, anapenda kuona naigiza, ananisapoti sana na hivi karibuni naachia kazi yangu mpya,” alisema Jack.

0 comments :

Post a Comment