Home » » FAMILIA ILIVYOBAMBWA IKILIMA UTUPU SHAMBANI

FAMILIA ILIVYOBAMBWA IKILIMA UTUPU SHAMBANI

Written By stephen kavishe on Wednesday, October 15, 2014 | 3:00 PM

MAAJABU ya mwaka! Watu wanne wa  familia moja, Makoye Kaboje, 42 (baba), Neema Kiwelu, 31 (mke) na watoto wao wawili (majina yapo) walikutwa wakilima shamba huku wakiwa watupu! Nyakati za saa 12 alfajiri katika shamba la familia huku wakiwa uchi.

Bwana Makoye Kaboje, 42 akiwa na mkewe Neema Kiwelu, 31 baada ya kunaswa.

Tukio hilo la aina yake lilijiri alfajiri ya saa 12, Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Bushingwana Kata ya Kalemila Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Tukio hilo ambalo mpaka sasa bado gumzo, liliwashangaza wengi wakidai kuwa ni mara ya kwanza kusikika katika mkoa huo mpya.Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wanaamini si mara ya kwanza kwa watuhumiwa hao kulima wakiwa hawana nguo, bali siku ya tukio walichelewa hadi jua linachomoza ndiyo maana walinaswa.
“Unajua wale wana kawaida ya kulima alfajiri ili jua likitoka wanaacha kwa kuvaa nguo na kuendelea kawaida. Sasa siku ile walijikuta wamepitiwa mpaka jua linachomoza wao bado, ndiyo maana walibambwa,” alisema mkazi mmoja bila kutaja jina.
Bwana Makoye Kaboje, akiwa na wanaye.
Uwazi lilipofanya mawasiliano na vyombo vya ulinzi na usalama hususan jeshi la polisi, lilikutana  na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Venance Kimario ambapo alifungukia kila kitu.
Msikie Kamanda Kimario: “Baada ya kukamatwa wakilima watupu shambani, walifikishwa kituoni kwa ajili ya mahojiano ambapo tulibaini kuwa, wote walikuwa wa familia moja na walikuwa  wanaongozwa na baba yao.
“Walisema kulima bila nguo ni mbinu mpya ambayo walipewa na ndugu yao mganga wa jadi kwa kuwa kufanya hivyo kutaongeza mazao, lakini hata hivyo, mganga huyo alifariki dunia mwaka jana kwa maradhi.”
Kaimu Kamanda Kimario alisema watuhumiwa wanashikiliwa katika Mahabusu ya Magu mkoani Mwanza kwa madai ya kufanya ushirikina hadharani.

0 comments :

Post a Comment