Home » » BABA: UMEME UMEMBADILI SURA MWANANGU

BABA: UMEME UMEMBADILI SURA MWANANGU

Written By stephen kavishe on Tuesday, October 7, 2014 | 2:00 PM

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14), mkazi wa Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Slaam amelalamikia umeme kubadili sura yake baada ya kuungua vibaya na moto uliosabishwa na hitilafu ya nishati hiyo katika nyumba yao iliyotokea wiki mbili zilizopita.
Kijana anayefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14) aliyeungua vibaya kutokana na hitilafu ya umeme.

Akizungumza na gazeti hili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji, baba wa kijana huyo Hussein Ally  alisema mtoto wake anayelala katika chumba karibu na dukani, alisikia vitu vikidondoka, lakini alipojaribu kuamka, akakutana na moto huo ukiwa umekolea.
Alisema kijana wake alitaka kuokoa mali zilizokuwa zinateketea na moto, lakini moshi na ukali wa moto ulimzidi nguvu na kusabisha kushindwa kuona na hivyo kuungua huku duka lote likiteketea.Alisema pamoja na mali zote zilizokuwepo dukani kuteketea, lakini pia mauzo ya siku 9 yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 1.9 nayo yaliungua.
“Kijana wangu ameungua vibaya sana, hapa ninamuomba Mungu tu maana hata kuongea ni shida,” alisema baba huyo kwa huzuni.Muuguzi aliyekuwa zamu, ambaye alikataa kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema kijana huyo ameungua vibaya, ingawa bado hawajajua ni kwa asilimia ngapi.
Saadam Hussein akiwa na Baba yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Kuna viwango cha kuungua, siwezi kujua ameungua kwa asilimia ngapi lakini  sehemu kubwa ya mwili wake umeuungua vibaya,” alisema.
Baba wa mtoto huyo alisema kijana wake alikuwa akifanya biashara hiyo kwa lengo la kuanza elimu ya sekondari ya binafsi na kutokana na kuungua kwa duka hilo, amebaki hajui la kufanya, wkani hata gharama za matibabu hospitalini hapo zinamtesa.
Aliwaomba watu wote walioguswa na kuungua kwa mwanaye kumsaidia kwa kutumia namba zake za simu ambazo ni 0786 89 51 14 au 0754 67 62 39.

0 comments :

Post a Comment