Home » » ANGALIA MAMBO WANAYOFANYA WASANII WA BONGO,KIOO CHA JAMII

ANGALIA MAMBO WANAYOFANYA WASANII WA BONGO,KIOO CHA JAMII

Written By stephen kavishe on Monday, October 6, 2014 | 3:15 PM


 
WASANII wa filamu nchini, Bond Bin Sinan na Salim Ahmed ‘Gabo’ hivi karibuni walinaswa wakisaga mirungi hadharani bila kujali kadamnasi.

Meza ya wasanii wa filamu Gabo na Bond ikiwa na dozi ya kutosha ya mirungi. Ishu hiyo ilitokea katika Ukumbi wa Dar West, Tabata Dar kulikokuwa na sherehe ya bethdei ya Wastara Juma ambapo wasanii hao walikuwa wamejaza mirungi kwenye mfuko wa nailoni na kuweka mezani huku wakitafuna kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shughuli.
Gabo aking'ata mirungi. “Duh! Jamani hawa wasanii wanakula mirungi hapa ukumbini ambako kuna watu kibao na wa aina mbalimbali hawaoni kwamba wanavunja sheria za nchi?” alisikika mmoja wa waalikwa.
Wenyewe walipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, hawakuwa tayari kujibu lolote zaidi ya kuendelea kutafuna.

0 comments :

Post a Comment