Home » » RAY C SASA ATAKA KUOLEWA NA MZEE!

RAY C SASA ATAKA KUOLEWA NA MZEE!

Written By stephen kavishe on Monday, September 29, 2014 | 7:44 AM

Utu uzima dawa! Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.

Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza kulea  mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.

0 comments :

Post a Comment