Home » » Picha: Rick Ross apost picha za Meek Mill akiwa gerezani

Picha: Rick Ross apost picha za Meek Mill akiwa gerezani

Written By stephen kavishe on Monday, September 29, 2014 | 12:00 PM


Rapper wa MMG, Meek Mill bado yuko jela akikamilisha kifungo cha kati ya miezi mitatu hadi sita alichohukumiwa July mwaka huu kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio ‘Probation’ kwa kosa la dawa za kulevya matumizi ya silaha mwaka 2009
.
Boss wa MMG,Rick Ross ameshare picha za rapper huyo kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kuwa atakuwa huru hivi karibuni kinyume na taarifa za awali zilizodai kuwa amezuiwa kutoka mapema.
Katika Picha moja, Meek Mill anaonekana akiwa amepoz na vazi la sweta akitabasamu kwa mbali. Na picha ya pili inamuonesha akiwa amekaa katika eneo la gereza na marafiki na familia.
“Meek in da building all OG’s roun’m.” Ameandika Rick Ross  na kuongeza, “Meek almost at the Door #FreeMeekMill Dreams Worth More than $$$$.

Kuhusu album ya Meek Mill ya ‘Dreams Worth More Than Money’ iliyokuwa imechelewa kutoka, Rick Ross amewathibitishia mashabiki kuwa itatoka hivi punde.

0 comments :

Post a Comment