Home » » MWIMBAJI AMTIMUA MWANAMKE!

MWIMBAJI AMTIMUA MWANAMKE!

Written By stephen kavishe on Monday, September 29, 2014 | 10:30 AM

Haijakaa poa! Katika hali isiyokuwa  ya kawaida, mwimbaji ambaye ni Prezidaa wa Bendi ya Mikumi Sound, Joshua Malekela amelazimika kumtimua mwanamke mmoja ukumbini, kisa kikielezwa ni mcharuko.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Black Poiny uliopo maeneo ya Iringa Road, Msamvu mjini hapa ambapo bendi hiyo ilikuwa ikishusha burudani.

Mlinzi akimuondoa mcharuko(jina halikufahamika) kutoka ukumbini.
Kabla ya kutimuliwa, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alikuwa akicheza ovyo na kuparamia waume za watu.

Pia kabla ya kutolewa, mwanamke huyo alionekana akikwidwa na shabiki wa bendi hiyo akimshutumu kujipendekeza kwa mumewe kwa kumlazimisha akacheze naye sebene huku akimwaga ‘lazi’ hadharani.
Mcharuko ukisindikizwa kutoka ukumbini.
Baada ya uongozi wa bendi kulalamikiwa juu ya mwanamke huyo, ndipo prezidaa huyo akaita mabaunsa na maafande wa ukumbi huo na kuwaamuru kumtoa nje mara moja, jambo ambalo lilitekelezwa.

0 comments :

Post a Comment