Home » » H. BABA NA MKEWE FLORA MVUNGI KUPEANA TUZO LIVE

H. BABA NA MKEWE FLORA MVUNGI KUPEANA TUZO LIVE

Written By stephen kavishe on Monday, September 29, 2014 | 4:00 PM

Baada ya kudai kunyimwa nafasi ya kupewa tuzo na waandaji wa tuzo mbalimbali nchini, H.Baba na mke wake Flora Mvungi, Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Giraffe Ocean View wanatarajia kupeana tuzo wao kwa wao.H.Baba amesema kuna mashabiki wao wengi wanapenda kuwaona wakipewa tuzo hali ambayo haijawahi kutokea.


“Hizi ni tuzo za kifamilia ambazo sisi tumeamua kupeana,” amesema. “Mke wangu mimi ni mwigizaji mzuri sana na mashabiki wengi wanampenda na wanajua uwezo wake katika tasnia ya filamu na mke wangu anatambua mchango wa H.Baba katika jukwaa, mambo ya performance na yeye kaamua kutoa ya kwake kwangu mimi.”


“Kwahiyo ni tuzo za wasanii lakini za kifamilia. Tunataka watu waone kwamba mashabiki wanahitaji waone watu wao wakipewa hivyo vitu lakini huwa hawapewi , sasa watu wanaamua kupeana wao kwa wao,” alisema H. Baba.

0 comments :

Post a Comment