Home » » CHEZEA KAJALA WEWE???? RAY, JB WAMPIGIA SALUTI

CHEZEA KAJALA WEWE???? RAY, JB WAMPIGIA SALUTI

Written By stephen kavishe on Monday, September 29, 2014 | 7:00 AM

Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti muigizaji mwenzao,  Kajala Masanja kutokana na filamu fupi aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na waandishi wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa  Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.
Kajala Masanja akiwa na mwanaye, Paula.
“Kitu ambacho nimekipenda ni kwamba filamu ni fupi lakini ujumbe umeeleweka pia amefikiri kitu cha tofauti kabisa kwani hata watoto wa rika zote wanaweza kuangalia kwa ajili ya kujifunza,” alisema JB huku Ray akiunga mkono hoja.

0 comments :

Post a Comment