Home » » SHILOLE, MCHUMBA’KE WAZICHAPA!

SHILOLE, MCHUMBA’KE WAZICHAPA!

Written By stephen kavishe on Friday, August 8, 2014 | 11:12 AM

Lile penzi lililopata ‘promo’ ya kutosha ndani ya muda mfupi kati ya mwanamuziki Zuwena
Mohammed ‘Shilole’ na Nuh Mziwanda limeingia shubiri baada ya juzikati wawili hao kuzichapa. Kisa cha wawili hao kuzibuana kinadaiwa ni baada ya Nuh kukuta sms tata ya mwanaume kwenye simu ya Shilole ambapo inadaiwa baada ya jamaa huyo kumtaka mchumba wake huyo ampigie aliyetuma meseji hiyo kukawa na kusuasua.
Mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Chanzo chetu cha habari kilichoomba jina lake lisichorwe gazetini kilitiririka: “Shilole na mchumba’ke walikuwa chumbani, mara ikaingia sms kwenye simu ya Shilole.
“Nuh alipoiona alimlazimisha Shilole ampigie jamaa aliyetuma sms na aweke ‘loud speaker’, Shilole alipoipiga ile namba, akajichanganya kidogo licha ya kuwa, jamaa alikuwa anamjua na wala hakuwa mpenzi wake ila ni washikaji tu.
Mwanamuziki na mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda akipozi.
“Kuona vile si Nuh akaanza kumpiga na hapo ndipo timbwili lilipotokea. Wote waliumia ila Nuh ndiye aliyeumia zaidi, ilikuwa ni vurugu kweli, baada ya ugomvi Nuh akaondoka na mfuko kama wa rambo hivi akiwa na vitu vyake kana kwamba katimuliwa,” kilidai chanzo hicho.Baada ya kuzipata nyeti hizo, Ijumaa lilimtafuta Nuh na alipopatikana alikiri kutokea kwa ugomvi lakini hakuwa tayari kuuzungumzia kwa kirefu.
Shilole alipopatika alisema: “Ni kweli tukio lilitokea. Ni hivi, aliyenitumia ile meseji ni mdau wangu, aliniambia kuwa yuko Dar tutafutane na wala si kwa mambo ya mapenzi lakini nikashangaa Nuh analazimisha nimpigie.
“Ile napiga naongea naye, si akanipiga kofi, hapo vurugu ikatokea. Kimsingi sikutarajia, ni kweli nampenda lakini mimi nadhani bora kila mmoja achukue hamsini zake.“Nilimheshimu sana, wamekuwa wakinitongoza wanaume wengi lakini nikawa nawakatalia kwa kuwa nampenda lakini leo anakuja kunipiga kwa mtu ambaye wala sina mpango naye. Amenikasirisha sana, acha aende zake, unajua mapenzi hayaendi hivyo,” alisema Shilole.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa, baada ya ugomvi huo Nuh alichukua kila kilichokuwa chake na kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na Shilole kwani alikuwa ni kama kahifadhiwa.

0 comments :

Post a Comment