Home » » SHAMBULIO LA ISRAEL KATIKA SHULE YA UN PALESTINA LAUA 10

SHAMBULIO LA ISRAEL KATIKA SHULE YA UN PALESTINA LAUA 10

Written By stephen kavishe on Monday, August 4, 2014 | 9:00 AM


Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza.
Mpalestina huyu akijaribu kuokoa maisha ya mtoto baada ya kushambuliwa na Israel leo.
Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akipelekwa kituo cha afya.
Baadhi ya Wapalestina wakilaani mashambulio yanayofanywa na Israel nchini huo huku miili na majeruhi ikiwa chini.
Majeruhi wakizidi kupatiwa huduma ya kwanza.
WATU 10 wamepoteza maisha huku 35 wakijeruhiwa baada ya shambulio la angani la Israel leo katika shule moja ya Umoja wa Mataifa iliyopo katika mji wa Rafah, Palestina.
Walioshuhudia shambulio hilo wanasema kuwa kombora lilipiga karibu na mlango wa shule hiyo. Kati ya waliofariki ni watoto na wanawake waliokuwa kwenye foleni kwa ajili ya kuchukua chakula.
Leo ni siku ya 27 tangu mapigano hayo makali kati ya Israel na Palestina kuanza ambapo jumla ya Wapalestina 1,700 na Waisrael 67 wamepoteza maisha mpaka sasa.
Shambulio hili limetokea baada ya siku nne tangu shambulio ligine kuua Wapalestina 15 waliokuwa katika shule ya Umoja wa Mataifa iliyopo Jabalya.

0 comments :

Post a Comment