Home » » MTOTO ANUSURIKA KUBAKWA KIBAHA

MTOTO ANUSURIKA KUBAKWA KIBAHA

Written By stephen kavishe on Wednesday, August 6, 2014 | 11:20 AM

Mtoto mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa) aliyenusurika kubakwa na njemba(Shukuru Abdalahman (49)).
MTOTO mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Kibaha amenusurika kubakwa na njemba inayofahamika kama Shukuru Abdalahman (49) anayeishi naye nyumba moja, asubuhi ya Julai 31, mwaka huu Kibaha Kwamatias.Akisimulia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Rashid alisema mtoto wake aliamka asubuhi na kuitwa na Shukuru chumbani kwake kwa madai ya kutaka kumtuma dukani, lakini alipoingia chumbani alifunga mlango na baadaye kumziba mdomo kwa vitambaa kumzuia asipige kelele.


Mama mzazi wa mtoto huyo, Bi. Amina Rashid.
“Baada ya kumtafuta kwa muda, nilikwenda chumbani kwa huyo baba, nikamkuta mwanangu amefungwa vitambaa mdomoni, nilipomuuliza kwa nini hali iko vile, akawa anababaika, nikamchukua mtoto na kumwambia baba yake, tukamuuliza kulikoni, akasema alitaka kuingiliwa kwa ahadi kwamba atapewa chokoleti na hela ya kutumia shuleni.
Baba wa mtoto aliyenusurika kubakwa.
“Tukamfuata na kumuuliza akakataa, tukaenda kwa mjumbe, alipoitwa baada ya kubanwa alikiri kutaka kumwingilia mtoto, akaomba yaishe kwa ahadi ya kutoa faini ya 30,000, lakini akatoa 20,000 kwanza, baba mtu akaenda Polisi kutoa taarifa,” alisema mama huyo na kudai kufunguliwa kwa faili lenye namba MKZ/RB/414/2014 KUJARIBU KUBAKA.
Njemba inayofahamika kama Shukuru Abdalahman (49) ikiwa kituo cha Polisi.  
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia njemba hiyo ambayo ilikuwa ikirejea nyumbani usiku kuogopa aibu na kukamatwa, akinaswa na na polisi na kupelekwa kituo cha Polisi cha Mkuza aliswekwa nyuma ya nondo kusubiri hatua zaidi za kisheria.

0 comments :

Post a Comment