Home » » MASTAA BONGO WAPEWA SOMO

MASTAA BONGO WAPEWA SOMO

Written By stephen kavishe on Saturday, August 9, 2014 | 3:00 PM

MWIGIZAJI wa filamu aliyekuwa akifanya shughuli zake katika nchi mbalimbali Afrika na Ulaya, Adili Matontu amewapa somo waigizaji wa Bongo kwa kuandaa kazi zenye ubora wa kimataifa.
Akizungumza na mwandishi wetu, Adili ambaye ni mtanzania, amesema kwa muda mrefu
amekuwa akilitazama soko la filamu Bongo likishindwa kuvuka mipaka na tatizo kubwa likiwa ni ubora wa kazi na uhalisia hivyo akaona aoneshe mfano kupitia sinema yake ya In Between.
“Ni vyema kwa wadau wa filamu nchini wakaitazama hiyo filamu ina vitu flani vya tofauti, kuanzia ubora na hata namna ambavyo imeandaliwa na washiriki kutoka Nigeria na Ghana,” alisema Adili.

Wanajeshi wakiwa kwenye roli wakati wa utengenezaji wa filamu.
Kwenye filamu hiyo yenye funzo kuhusu haki za binadamu, mbali na Adili kuwa muandaaji mkuu, imeongozwa na dairekta Pascal Amanfo kutoka Ghana, prodyuza Nkechi Destiny wa Nigeria na Emeka Amakeze wa Nigeria.

0 comments :

Post a Comment