Home » » KAULI YA DIAMOND PLATNUM KUHUSIANA NA SERENGETI FIESTA 2014 MKOANI MWANZA.

KAULI YA DIAMOND PLATNUM KUHUSIANA NA SERENGETI FIESTA 2014 MKOANI MWANZA.

Written By stephen kavishe on Sunday, August 10, 2014 | 11:00 AM


Mkali wa Mziki wa Kizazi Kipya hapa Bongo Diamond Platnum aka Rais wa Wasafi aka Dangote aka mahaba ninyote wa Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 tayari yuko Jijini Mwanza kwa ajili ya amsha amsha za Serengeti Fiesta 2014 ambayo inakata Utepe hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Akipiga Story ndani ya 99.4 Metro FM ya Jijini Mwanza hii leo, Platnum amebainisha kuwa kwa mara ya Kwanza atashusha burudani kali kwa wapenda burudani wa Mkoa wa Mwanza na Vitongoji vyake ikiwa ni katika Kufungua Msimu Mpya wa Serengeti Fiesta 2014 kwa mara ya Kwanza kabisa ikiwa inaanzia Kanda ya Ziwa ndani ya Mkoani MwanzaAmesema kuwa siku zote alikuwa akipanda jukwaani na madancers wane, lakini hii leo kwa mara ya kwanza atapanda jukwaaani na madancers 10 na atatumbuiza ngoma yake ambayo amesema inafanya poa sana katika ardhi ya Bongo kwa hivi sasa, ngoma ya mdogo mdogo.SOMA ZAIDI>>>

0 comments :

Post a Comment