Home » » WAHOLANZI 154 WAPOTEZA MAISHA KATIKA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOLIPULIWA NA KUUA 298

WAHOLANZI 154 WAPOTEZA MAISHA KATIKA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOLIPULIWA NA KUUA 298

Written By stephen kavishe on Friday, July 18, 2014 | 1:27 PM

Ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777-200 ikiteketea kwa moto baada ya kulipuliwa.

Mmoja wa waasi wanaoiunga mkono Urusi akiwa eneo la ndege iliyolipuliwa.
Waokoaji wakikagua katika mabaki ya ndege hiyo.
Baadhi ya miili ya watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyolipuliwa na kuanguka kijiji cha Grabovo kilichopo maili 30 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine.
Wananchi wakiweka maua katika eneo lililoandaliwa nje ya ubalozi wa Uholanzi huko Kiev, Ukraine.
Baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwa ndani ya ndege iliyolipuliwa.
Vikosi vya zimamoto vikipambana na moto uliokuwa ukiteketeza ndege ya Malaysia.
Waasi wanne wa Ukraine wanaoiunga mkono Urusi wakiwa eneo la ajali. Waasi hao ndiyo wanaodaiwa kuilipua ndege hiyo.
MAMLAKA nchini Uholanzi imesema kuwa watu 154 raia wa Uholanzi, 27 wa Australia na tisa wa Uingereza walikuwa miongoni mwa watu 298 waliopoteza maisha katika ndege ya shirika la Malaysia aina ya Boeing 777-200 yenye namba MH17 iliyolipuliwa mashariki mwa Ukraine jana.
Maafisa nchini Ukraine wamesema ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekea Kualar Lumpur ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo kwenye kijiji cha Grabovo kilichopo maili 30 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amelitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi huku Rais wa Urusi Vladimir Putin akiishutumu Ukraine kwa kutodumisha amani nchini mwake.
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miezi minne tangu ndege nyingine ya shirika hilo la Malaysia kupotelewa ndege aina ya Boeing 777-200ER iliyokuwa na namba MH370 ikiwa na watu 239 kutoka mataifa 14 ambayo mpaka sasa bado haijulikani ilipo.

0 comments :

Post a Comment