Home » » UKIMWI KUDHIBITIWA MWAKA 2030

UKIMWI KUDHIBITIWA MWAKA 2030

Written By stephen kavishe on Thursday, July 17, 2014 | 7:44 AM

Kuna uwezekano kuwa UKIMWI unaweza kudhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa.
Shirika hilo- UNAids- limesema idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya HIV na vifo vinavyotokana na UKIMWI inapungua.
Hata hivyo, imetoa wito kwa juhudi zaidi za kimataifa kwa kuwa "kasi ya sasa haiwezi kumaliza ugonjwa huo".
Shirika la Madaktari wasio na Mipaka limeonya kuwa wengi wa watu wanaohitaji dawa za kufubaza virusi vya HIV, bado hawawezi kuzipata dawa hizo.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa watu milioni 35 duniani kote wanaishi na virusi vya HIV.

Kulikuwa na maambukizi mapya milioni 2.1 mwaka 2013, asilimia 38 pungufu ya idadi ya milioni 3.4 mwaka 2001. Vifo vinavyotokana na UKIMWI vimepungua kwa humusi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na kusalia katika milioni 1.5 kwa mwaka. Afrika Kusini na Ethiopia zimeweza kupiga hatua kubwa. Sababu nyingi zinasaidia kubadili hali ilivyo, ikiwemo upatikanaji wa dawa. Kumekuwa na idadi mara dufu ya wanaume kutaka kufanya jando kama njia ya kupunguza hatari ya kupata au kusambaza virusi vya HIV.

0 comments :

Post a Comment