Home » » PICHA ZA KIPIGO CHA DIDA ZAVUJA

PICHA ZA KIPIGO CHA DIDA ZAVUJA

Written By stephen kavishe on Friday, July 4, 2014 | 8:36 AM

Picha zinazoonyesha jinsi mtangazaji wa kituo cha Redio cha Times, Khadija Shaibu alivyochezea kichapo kutoka kwa mumewe, Edzen Jumanne zimevuja.
Majeraha katika mwili wa Dida baada ya kipigo kutoka kwa mumewe Ezden.

Picha hizo zinamuonesha Dida akiwa na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mkononi, kichwani na mapajani.
Dida.
Akizungumzia kipigo hicho hivi karibuni, Dida alidai kuwa, baada ya kutofautiana kufuatia wivu wa kimapenzi, mume wake huyo baada ya kumporomoshea mitusi, alichukua mkanda wa suruali na kumpiga nao hadi kumsababishia majeraha hayo hali inayomfanya muda mwingi avae kininja kuficha aibu.
Dida akionyesha majeraha aliyoyapata.
Mpaka sasa wawili hao kila mmoja kivyake huku ndoa ikielezwa kuwa haipo tena.

0 comments :

Post a Comment