Home » » MAYA AIKACHA KANUMBA THE GREAT

MAYA AIKACHA KANUMBA THE GREAT

Written By stephen kavishe on Monday, July 14, 2014 | 7:22 AM

NDO basi tena! Staa wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa kwa sasa amejikita katika kupiga kazi za nje ya Kampuni ya Kanumba The Great Film hivyo asiulizwe kuhusu kampuni hiyo aliyofanya nayo kazi kwa muda mrefu.
Staa wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.

Akichonga na mwanahabari wetu, Maya alitiririka kuwa ameamua kuiweka kando kampuni hiyo na kujikita katika kazi za nje na ikiwezekana asimame mwenyewe.
“Nipo nje ya kampuni kwa sasa, kampuni inaongozwa na mama Kanumba (Flora Mtegoa) mwenyewe, nafanya kazi na watu tofautitofauti ili baadaye nisimame mwenyewe,” alisema Maya.

0 comments :

Post a Comment