Home » » MASTAA WA MUVI WAZICHAPA WAKIDAIWA.

MASTAA WA MUVI WAZICHAPA WAKIDAIWA.

Written By stephen kavishe on Monday, July 14, 2014 | 10:41 AM

Imevuja! Mastaa wawili wa kike Bongo Muvi, Vivian Minja na Najma wanadaiwa kutoleana maneno machafu kisha kuzichapa kavukavu chanzo kikidaiwa eti walikuwa wakimgombea Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movies, Steven Mengere.
Staa wa kike Bongo Muvi, Najma akiwa pembeni ya JB.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Vivian na Najma walifanya yao kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyokuwa wamealikwa na Steve iliyofanyika kwenye Mgahawa wa Great Wall ulipo Masaki, Dar.
Ilidaiwa kuwa wawili hao walianza kama utani lakini mambo yalipokolea, walijikuta wakipaza sauti kabla ya kudundana huku wakimtaja Steve Nyerere kuwa wote ni watu wake.

“Jamani Vivi na Najma wanagombea nini? Hapa kuna watu wanaojiheshimu, wao hawaoni wanadhani wako kwenye Viwanja vya Leaders (Kinondoni)” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa eneo la tukio.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walimwendea hewani Vivian ambaye alikiri kutokea kwa ugomvi lakini hakupigana.

Staa wa kike Bongo Muvi, Vivian Minja(kulia) akiwa na Davina.
“Kweli ugomvi ulitokea, kwani maelewano yalivurugika kidogo na sababu kubwa ilikuwa ni Najma kutajataja jina langu lakini mambo ya kumgombea Steve si kweli watu wamezusha,” alisema Vivian.
Kwa upande wake Najma alikuwa na haya ya kusema: “Vivi ndiye aliyeanza kunitukana na mimi sijazoea kugombana na watu kwa sababu ninajiheshimu, nikawa namfuata watu wakanishika, mimi sijawahi

kutembea na Steve na siwezi kutembea naye, ninajua vizuri tabia za Bongo Movie za kuzungukana wao kwa wao, siwezi kuwa naye kwa sababu wanaume matajiri wanaomtuma na kukaa nao mezani mmojawapo yupo mpenzi wangu ambaye ananiweka mjini.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi Steven Mengerem, 'Steve Nyerere'.
Baada ya Vivian kuzungumza, Steve Nyerere alimpigia mwandishi wetu na kudai kuwa yeye alikwenda kuwapatanisha na kuzuia kugombana kwa sababu yeye kama kiongozi ni kazi yake kufanya hivyo.
“Hivi nitakuwa na akili gani kuwaita wanawake wawili ambao ninatoka nao sehemu moja? Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho kwani nina familia yangu,” alisema Steve Nyerere.

0 comments :

Post a Comment