Home » » MAKALIO YA KOLETA YADATISHA WATU MLIMANI CITY!

MAKALIO YA KOLETA YADATISHA WATU MLIMANI CITY!

Written By stephen kavishe on Friday, July 18, 2014 | 9:53 AM

Msanii wa filamu, Coletha Raymond ‘Koleta’ hivi karibuni aliibua gumzo maeneo ya Mlimani City jijini Dar kutokana na kivazi alichokuwa amevaa huku makalio yake yakionekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Tukio hilo lilitokea juzikati wakati  Koleta alipokuwa akitoa kwenye lango kuu kuelekea ilipo ‘parking’ ya magari akiwa na mwanaume aliyeonekana kama mpenzi wake.

Msanii wa filamu, Coletha Raymond ‘Koleta’

Wakiwa katika eneo hilo, wawili hao walionekana wameshikana mikono huku mdada huyo akitembea kwa mikogo na kudeka, akichezesha makalio yake hali iliyoibua minong’ono.
“Mh! Huyu si yule Koleta muigizaji, haya makalio yake daah! Au kishatumia Mchina maana…!” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa akimsindikiza kwa macho huku wengine wakiendelea na mjadala juu ya kisuruali alichovaa na mwanaume aliyekuwa naye kama ni mpenzi wake ama laa.

0 comments :

Post a Comment