Home » » MAJANI, PROFESSOR J NA DIAMOND WAINGIA STUDIO UPYA KUIONEGESHA ‘KIPI SIJASIKIA’ KWAAJILI YA VIDEO

MAJANI, PROFESSOR J NA DIAMOND WAINGIA STUDIO UPYA KUIONEGESHA ‘KIPI SIJASIKIA’ KWAAJILI YA VIDEO

Written By stephen kavishe on Tuesday, July 22, 2014 | 8:30 AM

Itakapotoka video ya wimbo wa Professor J ‘Kipi Sijasikia’ aliomshirikisha Diamond Platnumz, unaweza ukasikia sauti mpya ambazo hukuzisikia awali kwenye wimbo huo uliotoka miezi kadhaa iliyopita.

10560953_512792668822216_699963228_n

P-Funk Majani, DJ na binamu wa Diamond, Romy Jones na Profesa wakiwa ndani ya studio za Bongo Records
10508092_248037908727065_2144386543_n

Picha za set ya video hiyo
Akiongea na East Africa Radio hivi karibuni, Professor alisema Diamond alijisikia kufanya marekebisho kwenye wimbo huo hivyo watu wategemee vitu vizuri zaidi kwenye video. “Audio tunakubali imeshatoka na imekubalika lakini video bado ina nafasi ya kuweza kuwekewa chochote kinachoweza kuboreshwa zaidi. Kwahiyo tunaweza kuboresha zaidi kwenye video kupitia audio kwasababu producer tunaye na anatuonesha ushirikiano kwa asilimia kubwa.”

10513936_255585301305768_934768718_n

Professor na Diamond wakiwa location kushoot video hiyo
Video hiyo imeongozwa na Adam Juma.

Source:BONGO5.COM

0 comments :

Post a Comment