Home » » KAN'TANGAZE: MAMA'KE DIAMOND ANASWA NYUMBANI KWA WEMA

KAN'TANGAZE: MAMA'KE DIAMOND ANASWA NYUMBANI KWA WEMA

Written By stephen kavishe on Monday, July 14, 2014 | 8:03 AM

KANTANGAZE! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi picha za tukio la Beautiful Onyinye, Wema Sepetu akiwa na ‘mkwewe’, Sanura Kasimu ‘Sandra’ wakiwa pamoja nyumbani kwa staa huyo wa filamu Bongo, Kijitonyama jijini Dar.
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu akimnawisha Diamond Platinum kwa ajili ya kupata futari.
Kwa mara ya kwanza, Sandra ambaye ni mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, alitia timu nyumbani hapo Ijumaa iliyopita kuitikia mualiko wa staa huyo kufuturu pamoja na kumkaribisha rasmi mwandani wake, Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani kushiriki tuzo za BET.
Diamond akiwa na baadhi ya washikaji zake kabla ya futari, pia Meneja wake, Babu Tale akiwepo.
MAHABA NIUE
Kuonesha kwamba mapenzi ni motomoto, wakati wa kufuturu, Wema alionekana akiwa bize kumhudumia zaidi mwandani wake huyo kila dakika na hata pale alipomaliza kula alionekana kumuwahi kabla hajanawa mikono na kumnawisha....Baadhi ya wageni waalikwa kwenye futari hiyo.
MABUSU MFULULIZO
Kama hiyo haitoshi, baada ya zoezi la kufuturu kukamilika mishale ya saa mbili, Diamond alimuita Wema ambaye alikuwa sebuleni na kwenda chemba kidogo wakioneshana malovee kwa mabusu motomoto mfululizo.

Wema na mpenzi wake Diamond wakiwa ni wenye furaha isiyo kifani.
Baada ya watu wengi kushangazwa na mabusu hayo na kuhoji uhalali wa swaumu yao, mapaparazi wetu walimuuliza Diamond kuhusu tukio hilo ambapo aliangua kicheko na kujibu kwa kifupi
“Daah! Seriously ni kipindi kirefu kidogo nimekuwa mbali na ‘baby’ jamani hivyo nimemmisi kupita maelezo. Siku ya leo nina furaha mno acheni tu, kwanza ni siku nzuri ya Ijumaa halafu nimekaribishwa futari na ‘baby’ wangu,” alisema Diamond.

Wema akideka kwa mkwe wake mama Diamond.
WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema hakuweza kufafanua kwa kina sababu za kufanya hivyo kipindi cha mfungo huku akiishia kuangua kicheko na kueleza kuwa kila anapomuona Diamond huwa furaha inamzidi.
“Kila ninapomuona huwa najisikia furaha tu, maana nilimmisi kupita maelezo,” alisema Wema.

MAMA DIAMOND AJIACHIA NA MKWEWE
Baada kufuturu, mama Diamond alionekana chumbani kwa mkwewe wakijiachia kwa raha zao kama ishara ya kumkaribisha mzazi huyo ambaye hajawahi kufika hata mara moja nyumbani hapo.
Ilielezwa kuwa wengi walishangazwa na tukuo hilo kufuatia wawili hao kudaiwa kutokuwa na mawasiliano mazuri kipindi cha nyuma hivyo kukata kilimilimi cha wapambe nuksi wasiopenda mafanikio ya penzi lao.

Mama Diamond ambaye huzungumza kwa kauli kama za vijana wa sasa, alisema kwa sasa hataki mbwembwe zozote na badala yake anamuomba Mungu ampatie mjukuu kutoka kwa Wema na mwanaye. 

0 comments :

Post a Comment