Home » » KANISA LAFUNGWA!

KANISA LAFUNGWA!

Written By stephen kavishe on Monday, July 21, 2014 | 10:31 AM

JAMBO limezua jambo! Kuhusu kilichotokea baada ya yule baba mchungaji wa Kanisa la Living World Ministry lililopo Ukonga-Majumba Sita jijini Dar, Michael Semeni kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu ni kwamba kanisa hilo limefungwa.
Baba Mchungaji wa Kanisa la Living World Ministry lililopo Ukonga-Majumba Sita jijini Dar, Bw. Michael Semeni mara baada ya fumanizi.

Habari ya mchungaji huyo iliandikwa na gazeti hili lenye uthubutu wa kuanika maovu bila kujali mhusika ana cheo gani, wiki mbili zilizopita ikiwa na kichwa ‘HEE! BABA MCHUNGAJI!’
Katika habari hiyo ilielezwa kwamba baba mchungaji huyo alikuwa akitaka kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mtu baada ya mwanamke huyo kwenda kanisani hapo kupata maombi maalum ya deliverance ili apate mtoto.

Bw. Michael Semeni alivyochukuliwa na kachero wa OFM mara baada ya fumanizi.
Ilidaiwa kwamba mara baada ya waumini au kondoo wake kuona picha na habari ya baba mchungaji huyo gazetini walisusa kwenda kanisani hapo.
Muonekano wa ndani wa kanisa hilo la Living World Ministry.
Habari zilizonaswa kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja (jina linahifadhiwa) zilidai kuwa baba mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo.
“Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa mtumishi wa Mungu. Baada ya gazeti kuwa mitaani baba mchungaji  hajaonekana tena na kanisa limefungwa,” alisema mmoja wa waumini hao bila kujua kuwa anazungumza na OFM

0 comments :

Post a Comment