Home » » HAUSIGELI MIAKA 8 AJERUHIWA NA BOSI WAKE

HAUSIGELI MIAKA 8 AJERUHIWA NA BOSI WAKE

Written By stephen kavishe on Tuesday, July 15, 2014 | 8:00 AM
Mtoto Miseto (8), anayedaiwa alikuwa akifanya kazi za ndani kwa mama mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mary Jerald mkazi wa Kijiji cha Busurwa, Wilaya ya Rorya, mkoani Mara ameokotwa ufukweni mwa Ziwa Victoria Juni 28, mwaka huu akiwa amejeruhiwa na anayedaiwa ni bosi wake.
 
Mtoto Miseto (8) aliyejeruhiwa na anayedaiwa kuwa bosi wake.
Taarifa kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo, Akeyo Thomas ambaye ni mchuuzi wa samaki katika
maeneo hayo alidai kwa wakati akiwa na wachuuzi wenzake walimuokota mtoto huyo akiwa amelala juu ya mchanga ufukweni mwa ziwa hilo huku akiwa na majeraha mbalimbali mwilini.
Akizugumza na mwandishi wetu wiki iliyopita kwa njia ya simu na kuthibitishwa na mmoja wa askari wa Kituo cha Polisi cha Busurwa,  alisema siku hiyo saa 12 asubuhi walimuona mtoto akiwa amelala juu ya mchanga huku akiwa na rundo la nguo ambazo alidai aliambiwa na bosi wake azifue.
“Tulimuuliza mtoto huyo sababu za kuwa na majeraha, akajibu kuwa amejeruhiwa na bosi wake anayeitwa Mary,” alisema Thomas.

Mtoto Miseto akiwa na jeraha utosini.
Aliongeza kuwa, walipomchunguza walimkuta na majeraha makubwa kichwani, mikononi na sehemu zingine za mwili huku akiwa amedhoofu kutokana na njaa.
“Tuliamua kumchukuwa na kumpa chai na maandazi, tukampeleka kituo cha polisi akafunguliwa jalada la kesi namba NYG/RB/52/2014 ambapo alipelekwa hospitali, baadaye bosi wake alikamatwa,” alisema Thomas.

Polisi wa kituo hicho wamethibitisha kukamatwa  bosi wa mtoto huyo, hata hivyo, hawakuwa tayari kueleza chochote kwa madai kuwa wao siyo wasemaji. 

0 comments :

Post a Comment