Home » » HAUSIBOI ALIVYOKULA UBONGO WA MTOTO

HAUSIBOI ALIVYOKULA UBONGO WA MTOTO

Written By stephen kavishe on Tuesday, July 22, 2014 | 9:18 AM

YALE mauaji ya kutisha ya mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) aliyeuawa kwa kucharangwa mapanga  kichwani hadi ubongo kutawanyika na kuliwa na mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22) ambaye naye alijikata uume pia akaula, akafa, bado yanatikisa nchi.
Mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22) aliyemuua mtoto wa bosi wake na kumla ubongo.

Tukio hilo la kutisha ambalo limeutetemesha vilivyo Mkoa wa Kilimanjaro, lilijiri Julai 18, mwaka huu saa 1:20 asubuhi nje ya nyumba ya baba wa mwanafunzi huyo katika Kijiji cha Samanga, Kata ya Marangu Mashariki.
MASHUHUDA, BABA MZAZI
Uwazi lilizungumza na baba wa marehemu Francis, Fortunatus Urassa pamoja na watu waliodai kushuhudia tukio hilo la kutisha.

Mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) aliyeuawa kwa kucharangwa mapanga.
Kwa mujibu wa baba huyo, mtoto wake alifikwa na mauti hayo muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kutoka shule ambako alisahau kitabu cha masomo. Marehemu alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Marangu Hills Academy.
Baba: “Baada ya kuingia ndani alimkuta muuaji akiwa chumbani, yeye akaenda kuchukuwa kitabu lakini ghafla muuaji alimfuata na kumfungia ndani na kuanza kumpiga.
“Kwa sababu mtoto wangu alipiga kelele, majirani walijitokeza, lakini muuaji aliwafukuza. Wakati huo tayari mwanangu alishaanza kulegea mwili kutokana na kipigo.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa akiwa hoi.
mfanyakazi wa ndani ‘hausiboi’, Lawrence Flavian (22)“Baada ya kuwatimua majirani, muuaji alimtoa mwanangu ndani na kwenda kutekeleza mauaji hayo kwa panga sasa katika shamba la mahindi ambalo lipo karibu na shule ikiwa ni umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwangu.”
SIKU MOJA KABLA YA MAUAJI
Kwa mujibu wa mzazi huyo, siku moja kabla ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alionekana kuchanganyikiwa akili kama ana mapepo lakini alifanyiwa maombi na kurejea katika hali ya kawaida hivyo kuondoa wasiwasi juu ya kile ambacho kilitokea.

Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kutisha.
MTUHUMWA ADAIWA KUUGUA KIFAFA
Mzee huyo aliendelea kudai kuwa, mtuhumiwa alikuwa mtu wa mikasa kwani mwaka jana alikumbwa na tatizo kama la kifafa mara tatu akatibiwa na kutulia.

MTUHUMIWA ALIKUWA MPOLE
Akieleza kwa undani juu ya maisha ya mtuhumiwa huyo, mzee Urassa alisema:
“Kwa kipindi cha miaka mitano ambacho nimekaa naye hapa nyumbani hajawahi kuonesha ukorofi wa aina yoyoye ile. Alikuwa msikivu, mwaminifu na mwadilifu lakini yametokea ya kutokea hatuna jinsi.”

'Hausiboi'(mtuhumiwa) akichukuliwa kutoka eneo la tukio. 
MASHUHUDA SASA
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wanaamini mtuhumiwa alirukwa akili, wakati marehemu Francis anapigwa walifika nyumbani hapo lakini mtuhumiwa aliwakimbiza, wakakimbia wakijua ni kipigo cha kumrekebisha mtoto ingawa haikuwa kawaida ya mtuhumiwa huyo kufanya hivyo.

Walisema baadaye wakagundua kuwa mtuhumiwa alitoka nje na mtoto huyo hadi kwenye shamba la mahindi ambako alimcharanga mapanga bila huruma kiasi cha kuutawanya ubongo wa mtoto huyo aliyekuwa na ndoto za kuwa rubani wa ndege.
ALA UBONGO, AKIMBILIA KICHAKANI
Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa, mtuhumiwa aliifikia hatua ya kuula ubongo huo uliokuwa umesambaa chini kisha akakimbilia kwenye kichaka jirani na nyumba kujificha ili asikamatwe.

Mmoja wa mashuhuda hao alisema, mtuhumiwa alimuua mtoto huyo wa bosi wake kwa kuanza kumpiga kwa panga kisha kumtoboa kichwani na ubongo ulipomwagika akauzoa kwa mikono na kunywa kama uji.
Marehemu mtoto Francis Fortunatus Urassa (9) enzi za uhai wake.
AKUTWA AMEJIKATA NYETI, AILA
Mashuhuda hao walisema walianza msako mkali na dakika chache baadaye walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amejikata nyeti na alikuwa akizitafuna kama nyama ya mshikaki.

JESHI LA POLISI LINAVYOSEMA
Akizungumza na Uwazi kuhusu mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Robert  Boaz alisema mtuhumiwa huyo alishikwa na mapepo.
Alisema mtuhumiwa alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospital ya Kilema, Moshi akiwa hajaanza kupatiwa matibabu. 

Mtoto Francis Fortunatus Urassa akiwa na marafiki zake enzi za uhai wake.
MAZISHI
Marehemu Francis alitazamiwa kuzikwa jana Jumatatu nyumbani kwa wazazi wake eneo la Shimbi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

NI MAUJI YA PILI
Haya ni mauaji ya pili ya kikatili kutokea katika kipindi cha miezi miwili mkoani Kilimanjaro ambapo hivi karibuni kijana Yusuf  Njau (32) mkazi wa Kijiji cha Masama-Roo  Kata ya Machame Mashariki Wilaya ya Hai aliwaua kwa shoka wazazi wake kisha kuchoma moto nyumba yao.

0 comments :

Post a Comment