Home » » DAWASCO WAONDOKA NA VIFAA VYOTE VYA MWENYE KIWANDA CHA KUFYATUA MATOFALI KIMARA ALIYEKAMATWA AKIIBA MAJI

DAWASCO WAONDOKA NA VIFAA VYOTE VYA MWENYE KIWANDA CHA KUFYATUA MATOFALI KIMARA ALIYEKAMATWA AKIIBA MAJI

Written By stephen kavishe on Saturday, July 26, 2014 | 2:00 PM

 Wafanyakazi wa kampuni ya Majembe Auction Mart wakifungua mashine ya kutengenezea matofali katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam.Wizara ya Maji iliamrisha kukamatwa kwa vifaa na mali mbalimbali za Martin Kessy aliyekuwa amejiunganishia maji kinyume na sheria na kufanya biashara ya kufyatua matofali.  Zoezi hilo linaendelea. Zoezi hilo limefanyika jana katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam jana.   .
 Mwenyekiti wa kamati maalum ya Wizara ya Maji, Eng. Hamis Blangson (kulia) akisikiliza jambo wakati
 wa operesheni maalum ya kupambana na watu wanaojiunganishia maji kinyume na sheria na kusababisha hasara kwa serikali na matatizo ya huduma hiyo kwa wananchi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Bw. Twaha Mohamed (kushoto) na Bw. Juma Maingu (katikati).  Zoezi hilo linaendelea
Kifaa cha kubebea vifaa vizito cha DAWASA kikiondoka na moja ya mashine ya kutengenezea kutengenezea matofali katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam. 

0 comments :

Post a Comment