Home » » ASKOFU TUTU AUNGA MKONO WAGONJWA MAHUTUTI WASAIDIWE KUFA

ASKOFU TUTU AUNGA MKONO WAGONJWA MAHUTUTI WASAIDIWE KUFA

Written By stephen kavishe on Thursday, July 17, 2014 | 7:13 AM

Askofu mstaafu wa Afrika Kusini Desmond tutu amesema kwamba anaunga mkono wagonjwa mahututi wanaotaka kusaidiwa kufariki wafanyiwe hivyo.
Akiandika katika jarida la 'The Observer'',alisema yeye anasheshimu utu lakini hali inaweza kubadilika.Pia alisema kuwa kuendeleza maisha ya Nelson Mandela ilikuwa kumvunjia heshima.
Maoni ya askofu huyo mstaafu wa kanisa la kianglikana, ni sawa na yale aliyetamka Askofu mkuu wa kanisa la 'Canterbury Lord Carey' ambaye pia aliunga mkono usemi huo.
Kanisa la kianglikana limeagiza uchunguzi kuhusu jambo hili.
Akiandika katika jadrida hilo, askofu huyu mstaafu wa kanisa la Anglikana Afrikakusini na mwenye miaka themanini na mbili alisema kwamba ''iwapo twahitaji mashine za kupumua,bila shaka tunahitaji kuuliza ubora wake na vile fedha zinavyotumika.''

Vile vile alieleza kuwa ni aibu vile aliyekuwa kiongozi wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliwekwa hai kwa mda mrefu hospitalini katika hatua za mwisho za maisha yake huku akipigwa picha na wanasiasa waliomtembelea.
Amesema kuwa Madiba hakujielewa kwa lolote na tendo lao lilikuwa ukiukaji wa heshima za hayati Mandela.
'Ni kweli kwamba watu watahuzunika iwapo nitasema nisaidiwe kufa lakini kwa kauli yangu binafsi sina shaka na hilo.''
Tutu aliandika kuwa,hata ingawa amebadilisha maoni yake,uhakika wa hapo awali hautiliwi maanani kwenye uhalisia wa mambo yalivyo a hasa kwa wagonjwa walio mahututi.

0 comments :

Post a Comment