Home » » AMANDA AANIKA SABABU ZA KUTOKUZAA

AMANDA AANIKA SABABU ZA KUTOKUZAA

Written By stephen kavishe on Thursday, July 10, 2014 | 10:26 AM


STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona mwanaume wa kuwa baba watoto wake.

Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila anashukuru kwa sasa amempata.
“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.

0 comments :

Post a Comment