Home » » KALAMA:NIMEMUACHA MKE, SIJAWAACHA WATOTO

KALAMA:NIMEMUACHA MKE, SIJAWAACHA WATOTO

Written By stephen kavishe on Monday, June 30, 2014 | 9:31 AM

Vipi kaka, mimi nakuomba unipe ushauri, ninatamani kweli kutoka  kimuziki lakini sijapata soko, nifanyeje? Tedy,0752813366
KALAMA: Nenda kwa Mamuu Store waliopo Kariakoo (Dar) wanashughulika na usambazaji wa kazi za muziki watakusaidia.

Kalama akiwa kwenye picha ya pamoja na Isabela Mpanda.

MALENGO
Kalama nini malengo yako ya baadaye kuhusiana na muziki na maisha yako binafsi? Salim Liundi, Dar, 0659601205
KALAMA: Kuwa mwanamuziki wa kimataifa zaidi na kuhusu kimaisha ni kuwekeza kwenye biashara tofauti.

ETI AMEZIDIWA NA CHIPUKIZI?
Kaka mbona upo kimya sana au ndiyo changamoto za wasanii wachanga wamekuja kuwafunika kabisa? Salumu Kabunda, Iringa, 0763236597
KALAMA: Kimya kingi kina mshindo, ninajipanga bado na nyimbo mpya kibao zitakuja, kuhusu wasanii wachanga kila mtu ana nafasi yake.

DINI NI KIKWAZO?
Eti Luteni nasikia unashindwa kumuoa Isabela (Mpanda), kisa ni dini? Msomaji, 0652672805
KALAMA: Hapana, tunajipanga kwanza hatutaki kukurupuka.

HISTORIA
Kaka Kalama naomba historia yako kwa ufupi, umesoma hadi wapi, umri, kabila na tofauti na muziki unafanya kazi gani nyingine? Swaum, Dodoma, 0769429458
KALAMA: Niliacha shule nikiwa kidato cha kwanza kwa sababu ya muziki, nje ya sanaa ninafanya biashara, nina umri wa miaka 33 na kabila langu ni Mzaramo.

Kalama akiwa mzigoni.
GANGWE MOBB VIPI?
Vipi kundi lenu la Gangwe Mobb lipo na vipi mbona siku hizi umekuwa kimya? Abely Majiko, Dodoma, 0758458965
KALAMA: Kundi lipo sema kila mtu anafanya kazi zake lakini ikitokea kazi ya kufanya pamoja kama kundi huwa tunafanya.

ETI NI MSALITI?
Kalama kwa nini umeamua kuisaliti ndoa yako pamoja na familia yako na kutembea na mwanadada Isabela, huogopi michepuko? Witho Mheluka, Dar, 0755085551
KALAMA: Sijaisaliti ndoa ila tuliachana na mke wangu ndiyo nikawa na Isabela.

YEYE NA ISABELA VIPI?
Nakuona muda mwingi Kalama unaongozana na Isabela hivi ni upendo au wivu unahisi ukimpa nafasi atafanya michepuko? Fungeni ndoa hata ya bomani tu. Mrs Abuu Machale, Moro, 0653358681
KALAMA: Ni upendo wa kweli, sawa tutafunga ndoa.

MAFANIKIO
Umepata mafanikio gani katika kazi yako ya muziki? Jose, Mwanza, 0757904855
KALAMA: Yapo mengi ila siwezi kuyaweka wazi yote, kikubwa sanaa imenifanya nimefahamiana na watu wengi sana.

VIPI KUHUSU BIFU?
Kaka Kalama wewe ni wa kitambo sana, unaongeleaje ishu ya mabifu ya wasanii? Pia inakuwaje wasanii wachanga wanawafunika ninyi wakongwe yaani hatuwasikii kabisa? Rich Boy, Tabora, 0759093909

KALAMA: Nawasihi wasanii wenzangu tuachane na bifu na badala yake tufanye kazi kwa ushirikiano na tupendane. Wasanii wachanga siyo kwamba wanatufunika ila huu ni wakati wao, huwezi siku zote kuwepo wewe tu.
Luteni Kalama katika pozi.
SKENDO
Kaka Kalama unajiepushaje na skendo pia ulimpataje Miss Ruvuma, Isabela Mpanda? Rejina Musa, Arusha, 0767909535
KALAMA: Ni kujiheshimu tu, kuhusu nilivyokutana na Isabela ni historia ndefu ila tulikutana Lindi ambako tulikwenda na kundi letu la Gangwe kufanya shoo mwaka 2002, tukaanza urafiki hadi kwenye uhusiano.

KAMUACHA MKEWE?
Kalama ina maana umemuacha kabisa mkeo na watoto? Maana mimi nakujua vizuri. Vai, Tanga, 0715282806
KALAMA: Nimemuacha mke, sijawaacha watoto.

\HUYU ANAMFAHAMU SANA
Kalama nakujua vizuri, tumemaliza darasa moja Shule ya Msingi ya Tandale-Magharibi (Dar) na ulikuwa unakaa Uwanja wa Fisi (Manzese), babu yako alikuwa na mashine ya kusaga nafaka. 0758828014
KARAMA: Ni kweli.

YEYE NA MALIPO NI NDUGU?
Kwanza napenda kazi yako, naomba kuuliza eti wewe na Malipo ni ndugu? Fatuma Juma, Dar, 0657892533
KALAMA: Ni mdogo wangu nikitoka mimi anafuata yeye.

VIPI HUDUMA KWA WATOTO?
Wewe Kalama watoto wako unawahudumia vipi na wako wapi? Mama Elvis, Dar, 0656334307
KALAMA: Wako shule Bukoba huwa nawatumia fedha, wakati wa likizo huwa naenda kuwaona au wanakuja Dar.

BIFU NA INSPEKTA VIPI?
Nafarijika sana kukuona ukiwa bado unakaza buti kwenye gemu, nini chanzo cha mtafaruku kati yako na Inspekta Haroun? Assanary, Mwanza, 0757212099
KALAMA: Hatuna mtafaruku wowote na hatujawahi kugombana.

YEYE NA LINAH VIPI?
Uliwahi kutoka kimalovee na Linah (Estalina Sanga) kabla ya kukutana na Isabela? Joseph, Dar, 0713221774
KALAMA: Hapana sijawahi.

HUYU ANATAKA KUJUA?
Kaka Luteni wewe ni mwenyeji wa wapi? Asha Sadiki, Tanga, 0655954760
KALAMA: Mimi ni mwenyeji wa Dar.

OA SASA
Luteni Kalama mimi nakukubali ila unatakiwa uoe, acha uwaluwalu. Neema, Arusha, 0754086622
KALAMA: Sawa nitaoa.

HUYU ANAHOJI
Kwa nini wasanii wengi hawaoi, Luteni Karama nakupongeza kuwa na watoto wawili, mastaa wengi hawana watoto wanapenda kuishi bachela. Nofedy Mtete, Iringa, 0787104390
KARAMA: Sijui kwa nini, asante kwa pongezi.

0 comments :

Post a Comment